Realtime blog statisticsRealtime blog statistics
Scanning..

EPISODE 1. UTAJIRI TULIOUPATA KWA SABABU YA WEMA WETU

Mwandishi: Dominick chuwa
Whatsapp:0787325447

Katika mkoa fulani ambao imebarikiwa kuwa na bahari nzuri yenye kule samaki na pia vipato kwa watu. Kulikua na kijiji kimoja ambacho shughuli yao kubwa ilikua ni uvuvi hivyo wengi wa watu wa kijiji kile walikua wavuvi. Basi katika kijiji kile walikua wavuvi walioishi kama rafiki na kama ndugu wote wakiwa wamejenga pembezoni mwa bahari kwa ajili ya kuvua samaki usiku na mchna. Wallifanya kazi kwa bidii wakitamani siku moja wanaweza kuwa zaid ya wavua samaki. Familia yao iliwategemea. Kwa kuwa weng wao waliku ni baba wa familia.katika kundi lile alkua bwana Cheche ambaye alikua na umbo la mraba minne akijaza kila sehemu na pia yeye kweny kuvuta nyavu alipnda sana kwa kuwa ana nguvu nying. Wa pili alikua bwana Kitambi, alikua ni mzee wa makoamo na mwenye busara na aliwapa ushauri wenzake kuhuusu uvuvi na lionesha kuwa yeye ni mkongwe kwenye uvuvi. Vilevile alikua bwana Kingo, alikua ni mtu ambae mtulivu sana hakupenda shari wala nini na kazi yake kubwa ilikua ni kuendesha boti na pia mda mwingne kusuka nyavu. Na pia alikua bwana Kipara. Bwana kipara alkua mpenda sifa sana yani akifanya kitu kizuri hupenda kila mwenzake ajue na yeye pia alipenda kuvuta nyavu. Wote hao walikua ni wavuvi waliojumuika ili kuleta nguvu moja.

****************
Siku moja waliingia baharini kama kawaida yao walichuku mtumbwi na kuanza kupiga makasia kwa ajili ya kuvua samaki. Lakini siku hiyo walijitahidi sana kutupa nyavu huku na kule lakini hawakuambulia kitu. Kwa kweli siku hiyo ilikua ni ya maajabu kwao kwa kuwa hawakuwahi ata siku moja kukosa samaki. Basi weng wao walichoka na kukata tamaa hasa hasa bwana kipara. Ila mzee mwenye busara Kitambi aliendelea kuwapa moyo kwa kuwa alijua fika lazima watapata samaki. Wakiwa wamesimama kwa umbali.Mara bwana CHECHE kwa umbali aliona mtu ameelea juu ya kitu huku akiwa amepoteza fahamu. Hakufahamu mara moja ni nani hivyo aliwaambia wenzake kile alichokiona na wote waligeuka na kuangalia. Looo hawakuamini kuona kile walichokiona mbele yao licha ya kiwa mbali ila waligundua kuwa alikua ni msichana kwa kuwa sehemu ya mwili wake ilikua inaonekana. Hawakujishauri sana walianza kugeuza mtumbwi ili kuelekea pale mwili ulipo hawakujua mapema kama amekufa au laaa
............... ITAENDELEA..........
© Haki Zote Zimeifadhiwa Simulizi Za Picha Na Irene Mchokozi | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top